Jumatatu 9 Februari 2026 - 23:00
Mapinduzi ya Kiislamu yaliwatoa Wairani kwenye ukandamizaji wa utawala wa Twa'ghuti na kuwafikisha kwenye “uhuru”

Hawza/ Naibu Mkurugenzi wa Hawza ya Ilimu ya Dini ya Qom, huku akisisitiza nafasi muhimu ya Mapinduzi ya Kiislamu katika kuiokoa Iran kutoka katika ukandamizaji wa kitamaduni na kidini wa enzi ya Taghuti, alisema: Mapinduzi ya Kiislamu yaliingiza nchi katika hatua mpya ya utukufu, ucha-Mungu na uhuru, na yaliandaa mazingira ya kutawala kwa maadili ya Mwenyezi Mungu katika jamii.

Kwa mujibu wa ripoti ya mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Hamid Maleki, Naibu Mkurugenzi wa Hawza ya Ilimu ya Dini ya Qom, katika mkusanyiko wa wafanyakazi wa Kituo cha Usimamizi wa Hawza ya Qom uliandaliwa kwa mnasaba wa kumbukumbu ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu katika Madrasa ya Ilimu ya Dini ya Imam Musa Kadhim (a.s), Qom, aliwapongeza kwa Siku za Mwenyezi Mungu za Muongo wa Fajr, na akayatambua Mapinduzi ya Kiislamu kuwa hatua muhimu katika historia ya kisasa ya Iran, akasema: Mapinduzi ya Kiislamu yaliitoa nchi hii kutoka katika mazingira ya ukandamizaji, ufisadi na kudhalilishwa dini katika enzi ya Twaghuti, na kuipeleka kwenye mazingira ya utukufu, ucha-Mungu, uhuru na utawala wa maadili ya Mwenyezi Mungu.

Akiashiria ulazima wa kukumbuka matukio makubwa ya Mwenyezi Mungu, alisema: Mwenyezi Mungu Mtukufu ametutaka tuzikumbuke Ayyamullah, na Muongo wa Fajr ni miongoni mwa mifano mikubwa ya siku hizo; muongo ulioanza tarehe 12 Bahman kwa kuwasili kihistoria Imam Khomeini (ra) na baada ya siku kumi za juhudi na kusimama imara kwa taifa la Iran, ulipelekea ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Naibu Mkurugenzi wa Hawza ya Ilimu ya Dini ya Qom, huku akisimulia kumbukumbu za ujana wake katika miaka 1357 na 1358 (Hijria Shamsia), alielezea hali ya kijamii na kitamaduni ya enzi ya utawala wa Pahlavi na kuongeza:
Katika kipindi hicho, alama za ufisadi — hasa vituo vya kuuza vileo — zilionekana zaidi katika miji kuliko misikiti, na hata kupata huduma za msingi katika siku za mapumziko kulikuwa na matatizo makubwa. Ukandamizaji ulikuwa kiasi kwamba watu hawakuthubutu kuhifadhi vitabu vya dini majumbani mwao, na upinzani mdogo tu dhidi ya serikali ulikabiliwa na hatua za kiusalama.

Akiashiria mabadiliko ya msingi ya mazingira ya kitamaduni ya nchi baada ya Mapinduzi, alisema:
Leo katika Jamhuri ya Kiislamu, vyombo vya habari, redio, televisheni na vituo vya kitamaduni vimejaa mafundisho ya Qur’an na Ahlul-Bayt (a.s), na hii ni neema kubwa inayopaswa kuthaminiwa, hasa na kizazi cha vijana ambacho hakikuiona enzi hiyo; wanapaswa kujua Mapinduzi ya Kiislamu yalileta mabadiliko gani.

Hujjatul-Islam wal-Muslimin Maleki, huku akitaja nafasi ya wanazuoni wapiganaji katika ushindi wa Mapinduzi, alimkumbuka Shahidi Ayatullah Madani kama mfano mashuhuri na kusema:
Ikhlasi, ujasiri na roho ya kuwa pamoja na wananchi ya viongozi hao ndiyo iliyokuwa nguvu ya kusukuma Mapinduzi. Kumbukumbu za mapokezi ya wananchi kwa Imam Khomeini (ra) tarehe 12 Bahman zilionesha imani na mshikamano wa taifa la Iran ambao hauwezi kusahaulika.

Akiashiria kuendelea kwa njia hiyo yenye nuru katika zama za sasa, alisema: Leo pia Jamhuri ya Kiislamu inakabiliana na kambi ya dhulma na ubeberu wa kimataifa, na katika mstari wa mbele wa kambi ya haki kuna uongozi wa shakhsia kamilifu, mwanachuoni, faqihi, mpiganaji na mwenye ufahamu kama Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi, ambaye anaiongoza nchi kwa nguvu, hekima na ucha-Mungu.

Naibu Mkurugenzi wa Hawza ya Ilimu ya Dini ya Qom mwishoni, akisisitiza kuwa kufanya kazi katika taasisi ya hawza ni jukumu takatifu, alisema: Sote tuko katika nafasi iliyo chini ya uangalizi wa Imam wa Zama, Hadhrat Wali-Asr (a.j), na tunapaswa kuthamini tawfiki hii ya Mwenyezi Mungu.
Kutumikia katika taasisi inayomhusu Imam wa Zama (a.j) ni neema kubwa, na kumshukuru yeye ni kutekeleza wajibu kwa ikhlasi na uaminifu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha